Shule ya Sekondari ya Kilutheri Mwadui…Mwadui Lutheran Secondary School


 To read this document in English click here.

Mwadui Lutheran Secondary School (Shule ya Sekondari ya Kilutheri Mwadui) ni shule ya bweni kwa wanafunzi wavulana na wasichana. Shule hii inatoa elimu ya kidato cha kwanza mpaka cha nne na kidato cha tano mpaka cha sita. (Katika nchi ya Amerika, ni sawa sawa na high school na junior college.) Pia inafundisha maadili ya Kikristo kwa wanafunzi wote.

Eric Funke anafundisha katika maabara ya kompyuta mpya

Shule hii inaendeshwa chini ya uongozi wa Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania. Ina ushirikiano na Global Lutheran Outreach, Mwangaza Partnership for Education, Health, Family, and Faith, na washirika mbalimbali wa Kanisa la Kilutheri Missouri Synod Merekani. Mch. Yohana Nzelu ni mkuu wa shule. Kabla ya hapo shule ilikuwa serekali, ilikuwa shule ya Kilutheri 1996. Imo Mwadui ambapo mahali sawa ya Williamson Diamond Mine, shule inapokea wanafunzi wa imani mbalimbali.

Shule inajivunia kuwa na maktaba mpya ya kisasa.

Shule inafundisha masomo yote yanayopaswa yafundishwe  kutoka Wizara ya Elimu Tanzania (hisabati, fizikia, kemia, biolojia, historia, jiografia , uraia, biashara, bookkeeping, Kiingereza, Kiswahili), na pia masomo yasiyopaswa kufundishwa (kompyuta, ukulima, elimu ya Biblia). Imemaliza kujenga jengo jipya lenye chumba cha kompyuta chenye zaidi ya kompyuta 60 na maktaba kubwa.

Inajivunia kushiriki katika mpango masafa marefu (e-learning program) unaoitwa Studi Tanzania ambapo wanafunzi wanaweza kuangalia video na kufanya mazoezi yanayowasaidia kujifunza na kuboresha hisabati, fizikia, kemia, na biolojia.

Shule inatoa huduma ya ushauri nasaha na mshauri anaowasaidia wanafunzi ambao wanahitaji ushauri na kujifunza stadi za kusoma mambo ya shule. Inafanya masomo ya Pre-Form 1 na Pre-Form 5 na kuwasaidia wanafunzi kusoma waliomaliza shule za msingi au sekondari na kuwasaidia kujiandaa kuingia shule tena.

Shule hii inatambulika kama shule ya kwanza wilaya ya Kishapu na ya kumi na tano mkoa wa Shinyanga.

Kupata maelekezo ya kujiunga Kidato cha kwanza mpaka cha nne, bonyeza JOINING-INSTRUCTIONS-2016-FORM-ONE-FOUR (1)

Kupata fomu ya maombi ya kujiunga masomo ya Pre-Form 5 (Kabla ya Kidato cha Tano), bonyeza..OMU YA KUJIUNGA PRE FORM FIVE 2017.